Watumishi wa idara ya mapambo chini ya kitengo cha mapambo na miti katika shirika la Alkafeel, wameanza kupanda mauwa na miti ya aina mbalimbali katika eneo linalo zunguka kituo cha Alhayaat cha nne.
Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Ahmadi Mahmuud Atwawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Asubuhi ya Jumatatu watumishi wetu wameanza kuandaa eneo linalo zunguka kituo cha Alhayaat cha nne katika mji wa Hussein (a.s) wa kitabibu hapa Karbala, na wameanza kupanda miti ya mapambo na mauwa ya msimu na ya kudumu, ikiwa ni hatua ya kwanza ya upandaji miti”.
Akaongeza kuwa: “Hatua ya pili tutapamba kituo chote kwa ujumla pamoja na njia zake, ili kuweka mazingira yanayo mpa matumaini mgonjwa wa Korona, pamoja na kuweka miti ya vivuli na mapambo sehemu zote za kutolea huduma”.
Kumbuka kuwa kituo cha Alhayaat cha nne kipo katika hatua za mwisho, siku chache zijazo kitakabidhiwa kwa idara ya afya ya mkoa wa Karbala, kikiwa kimekamilisha sifa na vigezo.