Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya ufunguzi wa jengo la Alhayaat la nne la kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Karbala

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Jumapili ya mwezi (20 Dhulqaada 1441h) sawa na tarehe (12 Julai 2020m) imefanya ufunguzi wa mradi wa jengo la Alhayaat la nne, la kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu katika mkoa wa Karbala, baada ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho ndani ya muda mfupi na kwa ubora unao takiwa kulingana na mahitaji ya kituo, wajenzi ni kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na wametumia siku (25) kumaliza ujenzi huo, kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1000).

Jengo hili limeingia katika orodha ya majengo yaliyo kamilika na kuanza kutoa huduma kwa watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Najafu, kilicho jengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) na majengo mawili katika mkoa wa Karbala, kwenye mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu na kwenye hospitali ya Hindiyya, vituo hivyo vinapokea idadi kubwa ya watu walio ambukizwa virusi vya Korona hadi sasa, kazi ya kukamilisha majengo mengine matatu inaendelea kwenye mkoa wa Muthanna, Bagdad na Baabil.

Hafla ya ufunguzi huo imehudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Karbala pamoja na viongozi wa Atabatu Abbasiyya, wakiongozwa na katibu wao mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na wajumbe wa kamati kuu bila kumsahau mganga mkuu wa mkoa wa Karbala na kiongozi wa mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu.

Kumbuka kuwa kukamilika kwa jengo hili kumetokana na kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu, aliye himiza kusaidia sekta ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuwalinda wananchi na maambukizi ya virusi vya Korona, pia ni muongozo wa moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), aliye elekeza kujenga vituo vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona ndani na nje ya mkoa wa Karbala, hivi sasa ujenzi unaendelea kwenye vituo vingine vitatu vyenye ukubwa tofauti, kwenye mkoa wa Baabil, Bagdad na Muthanna.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: