Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) kinajiandaa kufungua jengo la (Yaasiin) litakalo tumika kuoshea watu waliokufa kwa janga la Korona.
Kiongozi wa kikosi kazi Sayyid Haazim Fadhili amesema kuwa: “Kazi iko hatua za mwisho, na tumesha anza kutoa maelekezo kwa kikosi cha uoshaji kutoka kitengo cha Dini”.
Akaongeza kuwa: “Zimebaki kazi ndogo kukamilisha kituo cha kuoshea maiti kwa ukamilifu”.
Akasema: “Kikosi cha uoshaji wa maiti kinahusisha majemedari wa Alkafeel na watafanya kazi mfululizo katika kuwahudumia wananchi wa Iraq, na kuwasaidia kuzika jamaa zao waliokufa kwa janga la korona ambalo tunamuomba Mwenyezi Mungu atuepushe nalo”.
Tambua kuwa mradi wa kujenga kituo cha kuosha watu waliokufa kwa janga la Korona, umetekelezwa kwa ufadhili wa Atabatu Abbasiyya, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, aidha ni sehemu ya kufanyia kazi maombi ya waumini, kikosi cha Abbasi kitachukua jukumu la kusimamia mazishi, sehemu hiyo imejengwa kwenye makaburi mapya ya Karbala, katika kiwanja chenye ukubwa wa mita (3750), chumba cha kuoshea maiti kinaukubwa wa mita (120), kinasehemu mbili, ya wanaume na wanawake, kinavifaa vyote vinavyo hitajika katika kumuosha mtu aliyekufa kwa Korona na kumpamba.