Kamanda wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) Maitham Zaidi, ametangaza kukamilika kwa kituo cha kuoshea maiti “Yaasiin” kimepewa jina hilo kwa ajili ya kutafuta baraka za Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w), sasa maandalizi yote ya kumzika mtu aliyekufa kwa janga la Korona yatafanywa katika Makaburi ya Karbala.
Yamesemwa hayo pembezoni mwa ziara ya Zaidi kwenye kituo hicho, akaongeza kusema kuwa: “Tumechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi wakati wa shughuli za maziko”.
Akaendelea kusema: “Mradi huu umetokana na maombi ya wananchi na kufanyia kazi maelekezo ya muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi”.
Akafafanua kuwa: “Tulichukua ruhusa kwa mkuu wa mkoa wa Karbala ambaye alielekeza idara ya ardhi pamoja na idara ya afya zionyeshe sehemu kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu, ujenzi huu umefuata taratibu zote za kiserikali na kiafya”.
Akasisitiza kuwa: “Kituo hiki ni maalum kwa ajili ya kushughulikia watu waliokufa kwa janga la Korona tu, pesa zote za ujenzi zimetolewa na Atabatu Abbasiyya”.
Akasema kuwa: “Kazi ya kuandaa maiti itafanywa bure, hatutapokea pesa yeyote kwani hili ni jukumu letu kisheria na kibinaadamu na kitaifa”.
Fahamu kuwa: “Viongozi wa kikosi cha Abbasi pamoja na viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu walikuwa watu wa kwanza kujitolea katika jambo hili la kheri”.
Akamaliza kwa kusema: “Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wataosha, kuvisha sanda na kuswalia jeneza pamoja na kuzika, kama aliyekufa anazikwa kwenye makaburi maalum ya watu waliokufa kwa Korona, au watasimamia mazishi kama aliyekufa ataenda kuzikwa kwenye makaburi ya kawaida”.