Kituo cha “Yaasiin” kimeanza kupokea miili ya watu waliokufa kwa janga la Korona

Maoni katika picha
Kikosikazi kilichoundwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) kwa ajili ya kufanya kazi kwenye kituo cha “Yaasiin” kimeanza kupokea miili ya watu waliokufa kwa Korona, kwa ajili ya kuwaosha na kuwapamba kisha kuwazika, shughuli zote zinafanywa bure kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wetu watukufu wa Iraq.

Mmoja wa wahudumu wa kikosi hicho bwana Hazim Fadhil amesema kuwa: “Katika kufanyia kazi maelekezo ya muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu, kikosi cha Abbasi leo kimeanza kuosha na kupamba watu waliokufa kwa Korona, baada ya kukamilisha ujenzi jana, akaonyesha moyo mkubwa wa kujitolea walionao majemedari wa kikosi cha Abbasi, kwani wanachukulia kuwa muendelezo wa jihadi yao ya kutumikia taifa hili”.

Tambua kuwa viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s), jana walitangaza kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kuoshea watu waliokufa kwa janga la Korona pamoja na kukamilika vitendea kazi vyote katika makaburi ya Karbala, sambamba na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi wakati wa shughuli za maziko, kitoa hiki kimejengwa kutokana na maombi ya wananchi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: