Ujenzi huu unafanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kusaidia idara ya afya ya mkoa wa Muthanna, kwenye eneo la hospitali ya shule ya Imamu Hussein (a.s).
Kazi inaendelea vizuri bila kusimama na imepiga hatua kubwa, kazi zinazo endelea hivi sasa ni:
- - Kuweka madirisha (PVC).
- - Kupaka rangi.
- - Kujenga dari.
- - Kuweka (PVC) kwenye vyumba vyote (114).
- - Kutengeneza mfumo wa maji kwenye vyoo vyote vya vyumbani.
- - Kupaka jipsam poda kutani (kuskim kuta).
- - Kufunga hita za kuchemsha maji kwenye kila chumba.
- - Kufunga mfumo wa zimamoto.
- - Kuweka marumatu vyooni pamoja na kukamilisha ujenzi wa vyoo vilivyokuwa bado.
- - Kufunga mitambo ya kuingiza hewa safi (AIR FRESH).
- - Kufunga umeme.
- - Kuweka ruva (tofali ndogondogo za chini) kwenye uwanja wa wazi mbele ya kituo.
- - Kazi ya kukata vyumba imesha kamilika kwa asilimia %100.
- - Ujenzi wa boma la chuma umesha kamilika kwa asilimia %100.
- - Ujenzi wa msingi umesha kamilika kwa asilimia %100.
Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo hiki unafanywa na kituo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, unakusudia kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa hospitali ya Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Muthanna, unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500), kikiwa na vyumba (114) vya wagonjwa, ujenzi unafanywa kwa matakwa ya wanufaika na kanuni za afya.