Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wapo kwenye hatua za mwisho katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha sita katika mkoa wa Muthanna, kinacho jengwa kwenye eneo la hospitali ya Imamu Hussein (a.s), wanatarajia kumaliza ujenzi ndani ya muda uliopangwa.
Mradi huo unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500) kinavyumba (114) vya wagonjwa, halafu kunavyumba vya madaktari, wauguzi, wahudumu na vyoo, kitasaidia kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa wa Korona, jengo hilo linajengwa kama lilivyo sanifiwa.
Baada ya siku chache ujenzi utakamilika na kituo kitaanza kutoa huduma, kazi zilizo bakia ni ndogo ngogo kama vile kupaka rangi baadhi ya vyumba, na kuweka urembo baadhi za sehemu, kutengeneza bustani, kuandika jina la jengo na kufanya ukaguzi wa mwisho kabla ya kukabidhi, ikiwa ni pamoja na (kufunga mitambo ya kuingiza hewa safi (AIR FRESH), kutoa hewa chafu, tahadhari, zimamoto, kamera, umeme na viyoyozi).
Kumbuka kuwa jengo la Alhayaat la sita katika mkoa wa Muthanna ni moja ya majengo matatu yanayo endelea kujengwa hivi sasa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye mkoa wa Bagdad na Baabil, aidha ni sehemu ya majengo manne yaliyojengwa, mawili katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu na moja katika hospitali ya Hindiyya mkoani Karbala, huku jengo la nne likijengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu, mradi huu ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia sekta ya afya kupambana na maambukizi ya Korona, na kuongeza uwezo wa kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.