Atabatu Abbasiyya tukufu na mkoa wa Muthanna Alasiri ya siku ya Alkhamisi mwezi (14 Muharam 1442h) sawa na tarehe (3 Septemba 2020m), wamefungua jengo la sita la kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Muthanna kilicho pewa jina la Shahidi Yusufu Najmi.
Kituo hicho kimejengwa kwa ufadhili wa wizara ya afya ya Iraq na mkoa wa Muthanna pamoja na michango ya wahisani, watekelezaji wa mradi huo walikuwa ni kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya vifusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa kupokea wagonjwa katika hospitali ya Hussein (a.s) mkoani Muthanna, kimejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500) kina vyumba vya wagonjwa (114) vimejengwa kwa kufuata matashi ya wanufaika na vigezo vya afya.
Kumbuka kuwa jengo la Alhayaat la sita katika mkoa wa Muthanna ni moja ya vituo vitatu vinavyo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya katika mkoa wa Bagdad na Baabil, aidha ni sehemu ya kukamilisha vituo vinne vilivyo jengwa siku za nyuma, viwili katika mji wa Hussein (a.s) na kimoja katika hospitali ya Hindiyya mkoani Karbala, na kimoja kilijengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu, vituo vyote ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi katika kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Korona.