Sayyid Swafi atembelea jengo la shule la kwanza na la tatu na amepongeza mafanikio yaliyo fikiwa

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi akiwa pamoja na katibu mkuu na rais wa kitengo cha miradi leo siku ya Jumamosi (1 Safar 1442h) sawa na (19 Septemba 2020m), ametembelea jengo la shule la kwanza na la tatu ambayo yamepiga hatua kubwa katika ujenzi wake.

Amesikiliza maelezo kuhusu ulipo fika ujenzi huo na kiwango cha ukamilifu wake, mwishoni mwa ziara hiyo amewapongeza watendaji wa mradi huo, kutokana na kazi kubwa waliyo fanya wakati huu wa mazingira magumu ambayo kazi nyingi zimesimama kutokana na janga la Korona, amesisitiza kuwa yupo tayali kusaidia jambo lolote litakalo leta maendelea katika sekta ya elimu hapa nchini na ujenzi wa shule ni kipaombele kikubwa kwake.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ziara hii ni moja ya ziara nyingi zinazo fanywa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha mradi huu ni miongoni mwa miradi muhimu inayopewa kipaombele zaidi, kutokana na matunda yake yanayo tarajiwa kwenye sekta ya malezi na elimu, ziara hizi zinatupa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa, na kuhakikisha tunakamilisha mradi kwa viwango vilivyo pangwa pamoja na mazingira kuwa magumu, hadi sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia %70 na bado kazi inaendelea”.

Kumbuka kuwa mradi huu unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m45,000) pia ni sehemu ya kukamilisha mfululizo wa miradi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya inayo lenga ujenzi wa shule za (msingi, sekondari na vituo vya utamaduni), ili kusaidia utowaji wa huduma ya elimu kwa kutumia njia za kisasa zinazo endana na wananchi wa Iraq bila kuingiliwa na tamaduni za kigeni ambazo zimeanza kuingia katika jamii ya wairaq, na kusaidia kulinda maadili ya kiislamu na mwenendo unaokubalika katika taratibu za kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: