Makamo katibu mkuu: Atabatu Abbasiyya tukufu itaendelea kusaidia watumishi wa afya kupambana na janga la Korona

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussawi amesema kuwa, Ataba takatifu inaendelea kusaidia wahudumu wa afya kupambana na janga la Korona, ujenzi wa vituo vya Alhayaat ni sehemu ya kuonyesha kwa vitendo mchango wetu katika vita hiyo, pamoja na mazingira magumu tuliyo nayo hayaja zuwia kufanya ujenzi huo, kituo hiki ni sehemu ya majengo saba yaliyo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo yamekamilisha sifa na vigezo vya kiafya.

Ameyasema hayo katika ufunguzi wa kituo cha Alhayaat cha saba katika mkoa wa Baabil, asubuhi ya Jumatatu (3 Safar 1442h) sawa na tarehe (21 Septemba 2020m), kilicho jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kama sehemu ya msaada wa kibinaadamu katika kuongeza uwezo wa kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.

Akaongeza kuwa: “Kituo hicho kimejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500) na kina jumla ya vyumba (99) vya wagonjwa, na vyumba (25) vya madaktari na wauguzi pamoja na watumishi wengine, kimejengwa na kukamilika ndani ya siku (54), miongoni mwa vitu vilivyopo katika kituo hicho ni mtambo wa Oksijen unao weza kuhudumia mita (36) kwa saa bila kuhitaji mitungi ya gesi, hali kadhalika imefungwa mifumo ya kisasa ya viyoyozi, umeme na vinginevyo, tunawashukuru sana waliotekeleza mradi huu, pamoja na ugumu wa hali ya hewa kutokana na kuongezeka kiwango cha joto na ukaribu wake na kambi ya wagonjwa wa Korona, wamefanikiwa kukamilisha ujenzi ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora mkubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: