Serikali ya Baabil imeishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha saba na imesema kitatoa huduma kubwa za kitabibu hapa mkoani

Maoni katika picha
Serikali ya mkoa wa Baabil imetoa shukrani na pongezi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha saba cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ambacho ni msaada mkubwa katika kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa hapa mkoani, na kusaidia wahudumu wa afya kupambana na janga la Korona.

Hayo yamesemwa katika ujumbe uliotolewa na msaidizi wa mkuu wa mkoa katika mambo ya kitaalam, Mhandisi Hamidi Ali Zarkani katika uzinduzi wa jengo la Alhayaat la saba ulio fanywa Jumatatu mwezi (3 Safar 1442h) sawa na tarehe (21 Septemba 2020m), jengo hilo limetolewa na Atabatu Abbasiyya kama zawadi kwa wakazi wa mkoa wa Baabil, nalo ni miongoni mwa majengo saba yaliyojengwa tangu kuwepo kwa janga la Korona, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu, aliye himiza kusaidia sekta ya tiba katika mazingira haya.

Akamaliza kwa kusema: “Tunashukuru watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu waliofanya kazi usiku na mchana na kuhakikisha wanakamilisha mradi huu ndani ya muda mfupi, tena kwa ubora mkubwa, hakika kweli ni majemedari wanaostahiki pongezi”.

Kumbuka kuwa mradi umejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500) jengo linavyumba vya wagonjwa (98) na vyumba zaidi ya (25) vya madaktari, wauguzi na wahudumu wengine, ni moja ya majengo saba yaliyo jengwa kwenye mikoa tofauti, kama vile Bagdad, Muthanna, na vituo viwili katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu, na kimoja katika hospitali ya Hindiyya mkoani Karbala, huku kituo kingine kikijengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu, vituo vyote ni sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu na muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) katika kusaidia sekta ya afya kupambana na janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: