Kwa maelekezo ya moja kwa moja kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, kimejengwa kiwanda cha kuzalisha Oksijen ya tiba katika hospitali ya Swadir mkoani Najafu, yamesemwa hayo na muwakilishi wake Sayyid Ahmadi Swafi ambae ni kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ili kuifanya hospitali hiyo ijitosheleze na Oksijen hiyo muhimu kwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona.
Dokta Adnani Kilabi mkuu wa kituo cha mafunzo ya tiba za mifupa na viungo vilivyo vunjika, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hii imefanywa kutokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Sistani tulipo kutana nae na kuzungumzia hali halisi ya afya hapa Iraq kwa ujumla na katika mkoa wa Najafu, ambapo alielezwa upungufu wa Oksijen mahospitalini, ikiwemo hospitali ya Swadir hapa Najafu, ndipo ofisi ya Mheshimiwa ikaitaka Atabatu Abbasiyya ijenge kiwanda hicho, nayo ikaanza mara moja ujenzi bila kuchelewa, leo hii tunazindua kiwanda hiki kitakacho ongeza uwezo wa hospitali katika kutoa huduma ya Oksijen”.
Kiongozi wa mambo ya tiba katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Osama Abdu Hassan amesema kuwa: “Tumechagua aina hii ya ujenzi wa kiwanda kutokana na mahitaji ja jengo na kinaweza kuendeshwa kielektronik, kinabomba maalum ya kusambaza gesi kwa kiwango kinacho hitajika na kituo”.
Naye Mhandisi Ali Nuru Razaaq kutoka kitengo cha miradi ya Atabatu Abbasiyya akasema: “Kiwanda hiki kimejengwa kisasa kwa viwango vya kimataifa, kina sehemu tatu za kuzalisha Oksijen, ambazo zinaweza kusambaza gesi ya Oksijen sehemu zingine, kwa kupitia (psa) na kuisafisha kwa kiwango cha juu kabisa, kila sehemu inauwezo wa kuzalisha mita (35) kwa saa”.
Akabainisha kuwa: “Kiwanda hiki kimejengwa nje ya hospitali na hakina athari yeyote, tumejengwa chumba maalum pembeni ya jengo na kuwekwa vifaa vyote vinavyo hitajika”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inamradi wa kujenga viwanda vya kuzalisha Oksijen, katika mkoa wa Dhiqaar ndani ya hospitali ya Hussein (a.s) na viwanda viwili ndani ya jengo la Alhayaat lililojengwa katika mkoa wa Baabil kwenye mji wa Marjana, viwanda vyote hivyo vinajengwa kutokana na maagizo ya Marjaa Dini mkuu ya kuhimiza kusaidia sekta ya afya kupambana na janga la Korona.