Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi huu unaendeshwa kwenye shamba lenye ukubwa wa (dunam 10,250), na tumepanda aina adimu za tende zinazo pamba vizuri na zinazo endana na ardhi ya Karbala, zikiwemo aina ambazo zilikua zimetoweka miaka ya hivi karibuni na taifa likaanda kuziagiza kutoka nje ya nchi, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kulima shamba la tende la mfano, nalo ndio msingi wa kuendeleza kilimo katika mashamba yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kurudisha heshima ya kilimo cha tende katika taifa hili tukufu.
Mkuu wa mradi huo Ustadh Zaki Swahibu akasema kuwa: “Hivi sasa tumeandaa shamba lenye ukubwa wa dunam (1000) zimegawanywa sehemu (25) na kupewa majina ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), kama vile shamba la Sayyid Auswiyaau, Khaatamu Ambiyaa, Sayyidat Fatuma Zaharaa (a.s), kazi ya kuingiza aina zingine bado inaendelea”.
Akafafanua kuwa: “Shamba hili lina zaidi ya aina ya tende adimu (95), kama vile (Balaka, Barim, Imrani, Shushi, Maktuum, Shukri, Khastwi, Makawi, Dakal-Halwa, Dakal-Hamza, Mirhaji, Mutwawwak, Tabarzal, Awidi, Saai, Shawishi, Ahmad na zinginezo..), wanatumia vifaa vya kisasa katika mradi huo wa kilimo sambamba na mbolea bora inayo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud, hadi sasa zimesha pandwa zaidi ya aina elfu (14) za tende, na kazi bado inaendelea”.
Akasisitiza kuwa: “Hatujaishia kulima tende peke yake, pali tumepanda miti ya matunda pia”.
Kumbuka kuwa lengo la kuanzishwa kwa shamba hili ni:
- - Kulinda heshima ya kilimo cha Iraq.
- - Shamba hilo ni kinga ya asili ya kuzuwia upepo na vimbunga vya udongo.
- - Ni fursa ya kuongeza ajira.
- - Kuingiza sokoni aina nzuri ya tende na adim.
- - Kutumia vizuri uwezo wa kilimo tulionao.
- - Kunufaika na maji ya visima.
- - Uwezekano wa kulima aina zingine za miti ya matunda.
- - Kuingiza vifaa vipya na mbinu za kisasa katika kilimo cha tende na kunufaika na uzowefu wa kitaifa na kimataifa.
- - Shamba hili kuwa msingi wa kupatikana kwa aina adimu za tende.
- - Kunufaika na jangwa na kulifanya kuwa eneo bora la kilimo.