Mradi wa ujenzi wa nyumba ya kulea watoto kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlulbait (a.s) umepiga hatua kubwa, tayali sehemu kubwa ya ujenzi imekamilika, watekelezaji wa mradi huu ambao ni kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kazi kubwa ya kukamilisha mradi huo ndani ya muda ulio pangwa na kwa ubora mkubwa.
Wapo katika hatua za mwisho, zinazo hitaji umakini mkubwa katika utendaji wake, haya yamesemwa na Mhandisi Muhammad Mustwafa Shaakir, akaongeza kuwa: “Hakika mafundi wanaotekeleza mradi huu wamefanya kazi kwa bidii kubwa na kufanikiwa kufika katika hatua hii ndani ya muda mfupi, jumla ya eneo la mradi ni (mt 400), jengo la ghorofa mbili, ghorofa la kwanza linavyumba sita, jiko na vyoo, ghorofa la pili lina kumbi tatu (3), vyumba vya ofisi na vyoo, aidha viyoyozi vya kisasa, mitambo ya zima moto na kamera zimewekwa kwenye jengo hilo.
Kumbuka kuwa mradi wa nyumba ya kulea watoto chini ya mafundisho ya Ahlulbait (a.s) ni moja ya miradi ya kijamii inayo fanywa na shule ya Darul-Ilmi ambayo ipo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajenga uwelewa wa kutambua turathi za Ahlulbait (a.s) kwa watoto, wanatumia vifaa vya kufundishia vya kisasa vinavyo muwezesha kuelewa kwa urahisi kila mtoto, siku za nyuma walikua wanatumia Husseiniyya na misikiti kufundishia, baada ya kupata muitikio mkubwa na kujitokeza watoto wengi ndio likaja wazo la kujenga kituo hiki cha kulea watoto.