Mradi wa firdausi wa shamba darasa la jangwani

Maoni katika picha
Idara ya maelekezo na mafunzo ya kilimo katika mkoa mtukufu wa Karbala, kupitia shamba darasa/ kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya kilimo cha shamba la Firdausi ambalo ni (moja ya mradi muhimu kimkakati katika Atabatu Abbasiyya), mradi huu unaonyesha namna ya kutumia umwagiliaji wa kisasa katika kilimo endelevu, shamba hili linatumiwa kuonyesha namna ya kutumia maji kwa njia za kisasa, na ndio teknolojia inayo tumika kwenye kilimo kwa sasa.

Tumejikita katika kuonyesha njia za umwagiliaji wa kisasa (umwagiliaji wa matone) pamoja na kubainisha aina za mbolea na utumiaji wake, na njia za kutumia dawa kwa uzalishaji wa mazao bora.

Tumeongea na Mhandisi Aadil Maliki mkuu wa shirika la Liwaau-Al-Aalamiyya linalo tekeleza mradi huo na msimamizi mkuu wa mradi amesema kuwa: “Tumetembelewa na kundi la wakulima wa majangwani, wakiwa pamoja na wawakilishi wa idara ya kilimo ya mkoa wa Karbala/ idara ya jangwani, wametembelea mradi na kuangalia vifaa vya kisasa vinavyo tumika kumwagilia sambamba na mfumo mzuri unao saidia kuboresha uzalishaji kwa kutumia maji kidogo”.

Akaendelea kusema: “Baada ya matembezi yao wameonyesha kufurahishwa na kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya kilimo kupitia mradi wa Firdausi, ambao ni mradi muhimu katika sekta ya kilimo hapa mkoani, tumewaambia kuwa Atabatu Abbasiyya ikotayali kushirikiana na yeyote kwa kubadilishana uzowefu na kusimama pamoja kutekeleza miradi inayoweza kusaidia kuboresha uchumi wa taifa, sambamba na kufanya miradi ya kutoa huduma”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: