Mradi wa ujenzi wa shule hatua ya kwanza na ya tatu unaendelea vizuri katika sekta zote kama ulivyo pangwa, uzuri wake umeanza kuonekana baada ya maendeleo makubwa yaliyo patikana katika hatua ya kwanza ya mradi huu uliopo kitongoji cha Ma’malaji katika mkoa mtukufu wa Karbala.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, akaongeza kuwa: “Huu ni miongoni mwa miradi yenye umuhimu mkubwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na mchango wake katika elimu kwa wanufaika”.
Kuhusu hatua za utendaji wa kazi tumeongea na Mhandisi Ali Hamiid msimamizi wa mradi huo kutoka kitengo cha miradi ya kihandisi amesema kuwa: “Mradi huu chini ya mkakati uliowekwa na kikosi kazi, hatua ya kwanza inahusisha ujenzi wa msingi na boma, hatua ambayo tayali imesha kamilika pamoja na uwekaji wa madirisha na milango sambamba na kupaka rangi”.
Akabainisha kuwa: “Kutokana na kukamilika hatua hiyo hivi sasa inaendelea kazi ya (tofali na rangi) nayo inakaribia kukamilika, tumemaliza hatua ya kwanza kwa ukamilifu, kuhusu kuweka mifumo mingine hiyo ni hatua ya umaliziaji, kama vile mfumo wa kutoa tahadhari, Intanet, kamera, redio ya ndani pamoja na mfumo wa viyoyozi na vyoo”.
Akafafanua kuwa: “Kazi ya ujenzi wa ukuta wa nje imefika hatua za mwisho, imekamilika kwa asilimia %90, huku kazi ya kuweka lami na kutengeneza njia ikiwa imefika zaidi ya asilimia %40”.
Kumbuka kuwa mradi huu unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (2m45,000) kuna jumla ya shule tano, kila moja imejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa mita (6000) na inaghorofa tatu, aidha kuna shule mbili za awali (chekechea) kila moja inaghorofa tatu, na kumbi mbili za michezo kila moja ikiwa na mita (900).