Mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitakatifu katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea na kazi ya kutengeneza dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) litakalo wekwa ndani ya ukumbi wa wanawake, baada ya kumaliza kutengeneza na kuweka dirisha kama hilo kwenye ukumbi wa wanaume.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya kwenye makaburi Sayyid Naadhim Ghurabi, akaongeza kuwa: “Mafundi wa kitengo chetu pamoja na kuwa na kazi nyingi lakini wameweka makadirio ya muda wa kumaliza kazi hiyo, kazi zote zinaendelea vizuri bila kuathiri kazi zingine, miongoni mwa kazi hizo ni dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), imefika hatua nzuri, tayali tumesha unganisha sehemu zote za umbo la mbao ambalo ndio msingi wa kuweka sehemu za madini, mbao zilizo tumika ni aina ya Burumi zenye ujazo unao endana na mzigo utakao wekwa”.
Akaendelea kusema: “Hakika dirisha hili linafanana na dirisha la upande wa wanaume, yanatofautiana vipimo tu, linaurefu wa (m3.80) na kimo cha (m2.95) na lina madirisha manne yanayo tenganishwa na nguzo yenye mapambo kila moja na nguzo nyingine ya msingi, halafu kuna mlango wa pande mbili zilizo ungana na dirisha, na kutenganishwa kwa ufito wa maandishi madogo yaliyo andikwa jina la kambuni iliyotengeneza na mwaka uliotengenezwa”.
Akasema: “Miongoni mwa kazi ambazo zinakaribia kuisha pia ni ufito wa maandishi ya shairi lisemalo (Ewe bwana wa mabwana ewe mtoto wa Mstwafa.. ewe hoja ya Mola kwako dahari imetosheka), nalo ni miongoni mwa mashairi yaliyo andikwa na Ali Swafaar Karbalai msaidizi wa makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, juu ya kila dirisha kuna ubeti mmoja, pamoja na ufito maalum wa maandishi ya Quráni yaliyo andikwa aya isemayo (Allah ni nuru ya mbinguni…) hadi: (…na likatajwa humo jina lake, vinamtakasa humo asubuhi na jioni), unao fuatiwa na ufito wa mapambo wenye urefu wa (m3.80) na kimo cha (sm32) ulionakishiwa mapambo ya mimea na mstari wa aya ya Quráni kazi ambayo pia inakaribia kukamilika”.