Utengenezaji wa dirisha la Magaam ya mkono wa kushoto umekamilika kwa asilimia %95

Maoni katika picha
Kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburini na milango mitakatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa mafundi wanaotengeneza dirisha la Maqaam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamekamilisha zaidi ya asilimia %90, kazi inaendelea kama ilivyo pangwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo hicho ustadh Husam Muhammad, akaongeza kuwa: “Kazi zinazo fanywa na mafundi wetu kwa sasa ni miradi mitatu, kwanza ni dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), pili dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) litakalo wekwa kwenye ukumbi wa wanawake, na mradi wa tatu ni dirisha la Maqam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi za miradi hizo zimegawanywa kwa kufuata utaratibu maalum na kuepusha muingiliano au mapungufu, hadi sasa utengenezaji wa dirisha la Maqam ya mkono wa kushoto umesha kamilika kwa zaidi ya asilimia %90”.

Akabainisha kuwa: “Sehemu iliyobaki ni baadhi ya maeneo ya ubavuni mwa dirisha, na mapambo ambayo yatawekwa sehemu ya juu ya dirisha hilo, kila sehemu moja ya dirisha inamapambo mawili yanayo tenganishwa na pambo la uwa, pamoja na taji la nguzo ambayo jumla yatakua nane, yote yatakua juu ya nguzo za dirisha”.

Akaendelea kusema: “Baada ya kumaliza kazi zote za kutengeneza umbo la mbao kwa ndani, tumeanza kupaka rangi sehemu zinazo hitaji rangi, kwa kuzingatia rangi ya kila sehemu ya dirisha, na kuzingatia uwekaji wa mina na maji ya shahabu kwenye maandishi ya mashairi na Quráni, na kweka ufito wa pambo juu ya maandishi hayo, kila sehemu inapambo, linalo kutana na pambo la sehemu nyingine”.

Kumbuka kuwa dirisha linaumbo la pembe nane, nalo ni dirisha la kwanza kutengenezwa kwa umbo hilo, linamzunguko wa mita natu (mt 3) na urefu wa (mt 2.85), limetengenezwa kwa silva yenye ujazo wa (mlm 2), limesanifiwa na kutengenezwa kwa umakini mkubwa, kazi hii inaingizwa katika orodha ya mafanikio mengo yaliyo patikana ndani na nje ya Iraq chini ya ufundi wa raia wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: