Rais wa uongozi wa Wakfu-Shia Dokta Haidari Hassan Shimri amesema kuwa miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inasaidia raia wa Iraq.. ameyasema hayo alipo tembelea mradi wa elimu uliochini ya Ataba tukufu, akiwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.
Akaongeza kuwa: “Miradi inayofanywa na Ataba tukufu, inamchango mkubwa katika sekta ya elimu kuanzia masomo ya awali hadi masomo ya juu”.
Akasisitiza kuwa: “Hakika hii ni miradi ya kitaifa, kimalezi, kibinaadamu na kimaadili, inamchango mkubwa katika jamii, naomba mamlaka za serikali zinazo husika zitoe ushirikiano unaostahiki katika miradi hii kwa faida ya taifa”.
Naye katibu mkuu wa Ataba tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar akasema kuwa: Hakika ziara ya Rais wa Wakfu-Shia katika miradi ya elimu ya Ataba tukufu, ni kwa ajili ya kuangalia mafanikio yaliyo patikana katika miradi hiyo muhimu, sambamba na ubora uliopo katika miradi hiyo.
Akasema: “Miradi hii inatoa ujumbe kuwa wairaq wanaweza kufanikisha mambo wakati wowote na kwa kiwango chochote”.