Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea mradi wa jengo la shule la kwanza na la tatu, kwa ajili ya kuangalia utendaji wake.
Katika ziara hiyo amefuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, Mheshimiwa amesikiliza maelezo kuhusu mradi huo kutoka kwa watendaji wa mradi, ambao wameeleza kiwango cha ukamilifu na hatua za ujenzi kitaalam.
Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ziara iliyofanywa na kiongozi mkuu wa kisheria ilikua na lengo la kuangalia hatua za mwisho katika mradi huo na kutoa maoni, kwani huu ni mradi muhimu kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, jengo hilo litakusanya taasisi zote za elimu kuanzia masomo ya awali (chekechea) na kuendelea katika mkoa wa Karbala, litaweka uwiyano katika mifumo ya malezi na elimu”.
Akaongeza kuwa: “Jengo hili linafuatiwa na jengo lingine ambalo limeanza kujengwa, moja litakua la wavulana na lingine la wasichana, yatatoa fursa kwa kitengo cha malezi na elimu ya juu kufanya shughuli zake katika majengo hayo, na kufikisha ujumbe wake pamoja na malengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kutumikia watu wa Karbala wanao jitokeza kwa wingi kusajili watoto wao katika shule za Al-Ameed tangu kuanzishwa kwa shule hizo miaka michache iliyopita”.
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni miongoni mwa miradi ya kimkakati unao simamiwa na kitengo chetu, tumetumia uwezo wetu wote kuhakikisha tunajenga jengo la kisasa litakalo wezesha kufikia kwa malengo ya kitengo cha malezi na elimu, tayali mradi huu umepiga hatua kubwa, utakua tayali kwa kupokea wanafunzi katika mwaka wa masomo ujao, sasa hivi tunakamilisha ufungaji wa umeme na tuanze kuweka vifaa kwenye kila chumba, ziara ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya ni kwa ajili ya kutoa maoni, na kuangalia kiwango cha ukamilifu pamoja na kushajihisha uongezaji wa juhudi kwa ajili ya kukamilisha sehemu iliyobaki”.
Kumbuka kuwa mradi huu unajengwa kwenye kiwanja kinacho kadiriwa kuwa na ukubwa wa (2m45,5000) panajengwa shule tano, kila moja inaukubwa wa mita (6,000) na itakua na maghorofa matatu, na shule mbili za awali kila moja itakua na ghorofa tatu na ukubwa wa mita (900), na kumbi mbili za michezo, kila moja utakua na ukubwa wa mita (900).