Chuo kikuu cha Al-Ameed kimezindua jengo la udaktari wa meno

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo siku ya Jumapili mwezi (21 Shabani 1442h) sawa na tarehe (4 Aprili 2021m) imezindua jengo maalum kwa ajili ya mchepuo wa udaktari wa meno.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi amesema: “Leo tunashuhudia uzinguzi wa mradi huu mtukufu, uliojengwa na watumishi wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Ataba tukufu”, akaongeza kuwa: “Mradi huu utanufaisha wanafunzi pamoja na jamii, utatoa huduma kwa bei nafuu”.

Naye mjumbe wa kamati kuu ya Ataba Dokta Abbasi Rashidi Mussawi akasema kuwa: “Mradi huu ni sehemu ya miradi ya Ataba tukufu ya kuboresha sekta ya elimu, kwa kuweka mazingira mazuri ya kujisomea kwa wanafunzi”, akasema: “Mradi huu ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Karbala, kwa sababu utatoa huduma kwa gharama ndogo sawa na bure”.

Mkuu wa chuo cha Al-Ameed Dokta Muayyad Ghazali amepongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kusaidia sekta ya elimu na kuendelea kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu fungua link ifuatayo:

https://alkafeel.net/projects/view.php?id=104
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: