Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, mafundi wa kitengo cha uhandisi walifanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kutumikia wananchi na kusimama pamoja nao katika mazingira hayo magumu.
Mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kitengo cha majengo ya kihandisi, walifanikiwa kujenga kituo hicho kilicho kidhi vigezo vya wizara ya afya ya Iraq, mafanikio hayo yalipatikana kutokana na vitu vingi, ikiwa ni pamoja na uwezo wa Ataba na watumishi wake ambao ni raia wa Iraq, kilijengwa na kukamilika haraka sana kushinda vituo vingine vilivyo jengwa katika kipindi hicho kigumu.
Jengo lipo katika eneo la mji wa Imamu Hussein (a.s) ndani ya mkoa wa Karbala, lilikamilika ndani ya siku (15) tu, linavyumba (60) na lipo kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (1550), miongoni mwa wasifu wa jengo hilo ni:
- - Ukubwa wa kiwanja ni mita (1550).
- - Ukubwa wa jengo ni mita za mraba (1365), vipimo vyake ni (mt26 x 52,5).
- - Sehemu ya kiwanja iliyobaki imetengenezwa bustani na sehemu za kutolea huduma.
- - Idadi ya vyumba vya wagonjwa ni (56), ukubwa wa kila chumba ni (mt4 x 3) vinaurefu wa (sm280), kila chumba kina choo, kitanda, kabati na meza.
- - Vyumba vya ofisi na dawa vipo vinne, kila kimoja kinaukubwa wa (mt6 x 3).
- - Jengo linapande mbili zinazo unganishwa na barabara mbili, upande wa barabara moja unaungana na kituo cha zamani.
- - Kila upande unaukubwa wa mita (551,25) na vyumba (28) vinavyo tenganishwa na njia ya katikati yenye urefu wa mita (49.5) na upana wa mita (3), pande hizo mbili zinatenganishwa na uzio wa katikati unao tazama upande wa madirisha, sehemu hiyo vimewekwa viyoyozi na hita za kuchemsha maji.
- - Jengo linamitambo maalum ya (air fresh) yenye uwezo wa kuuwa bakteria na kusafisha hewa, inavifaa maalum vinavyo iwezesha hewa ndani na nje yake.
- - Vifaa vyote vinavyo tumika ndani ya kituo vimekidhi vigezo vya wizara ya afya ya Iraq, na vinaendana na jengo hili.
- - Katika ujenzi wa kituo hiki tahadhari zote za kiufundi na kiafya zilizingatiwa, ikiwa ni pamoja na uwekaji wa njia za kuingia na kutoka, sehemu ya dharura, pia jengo linaweza kutumika kama hospitali ya kawaida baada ya kuisha janga la Korona.
- - Umezingatiwa utoaji wa huduma za afya unao endana na jengo hili, na kuunganishwa na mfumo wa hospitali.
- - Sehemu lilipojengwa ilichaguliwa kwa kuzingatia misingi ya uhandisi wa majengo, inafikiwa na mionzi ya jua pamoja na hewa safi, wala haitatizi huduma zinazo tolewa na mji wa Hussein (a.s) wa kitabibu, jengo la (Alhayaat) la pili ni jipya.
- - Jengo limefungwa taa zinazo endana na maeneo husika, sawa iwe ndani ya chumba, au kwenye korido na zinaweza kutumika kadri ya mahitaji.
- - Jengo limefungwa mitambo ya tahadhari na zima moto inayo endana na mazingira ya kituo.