Majengo ya shule yametimiza masharti ya kufaulu katika mpango wa kimkakati

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa ujenzi wa shule ya kwanza na ya tatu, unaendelea vizuri katika hatua zote kama ilivyo pangwa, tumekamilisha masharti mawili ya kimkakati yanayo husu sekta ya malezi na elimu, nayo ni ubora wa majengo na mazingira.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shirika linalo tekeleza mradi limefanikiwa kukamilisha kiwango kikubwa cha ujenzi, na linatarajia kumaliza kazi ndani ya muda uliopangwa, pamoja na uwepo wa mazingira magumu kiafya na uhaba wa pesa, kiwango cha ukamilifu kinakaribia asilimia (%85), sehemu kubwa ya kazi zilizo baki ni za umaliziaji, pamoja na kukagua mitambo iliyo fungwa ndani ya jengo”.

Akaongeza kuwa: “Hatua ya kwanza pia imepiga inaendelea vivuri, hadi sasa imefika asilimia (%45), kazi hiyo inahusu ujenzi wa sehemu ya chini na njia kuu na ndogo pamoja na kazi zingine”.

Kumbuka kuwa mradi huu unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m45,000), kuna majengo ya shule tano, kila shule inaeneo lenye ukubwa wa mita (6000) kuna majengo matatu ya ghorofa, na kuna shule za awali mbili kila moja ikiwa na jengo la ghorofa tatu, kila moja likiwa na ukubwa wa mita (900) na kumbi mbili za michezo, kila mmoja ukiwa na ukubwa wa mita za mraba (900).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: