Kazi ya kuweka Kashi karbalai kwenye mlango wa Imamu Hassan (a.s) kwa ndani imekamilika kwa asilimia %90, bado kazi inaendelea kukamilisha sehemu iliyobaki, inatarajiwa kukamilika kabla ya ziara ya mwezi kumi Muharam.
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza kuweka marumaru kwenye ukuta wa ndani wa mlango wa Imamu Hassan (a.s), ambao ni miongoni mwa milango muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hivi sasa tunaweka Kashi Karbalai iliyotiwa dhahabu pamoja na nakshi tofauti, hizi ni kazi za mwishomwisho katika mlango huu, baada ya kukamilika kazi nyingi za awali”.
Akaongeza kuwa: “Baada ya hapo kazi itaendelea kama ilivyo pangwa ya kuweka nakshi na mapambo kwenye paa, inatakiwa kufanywa kwa umakini na ujuzi mkubwa, maandalizi ya kazi hiyo yamesha kamilika kwa kiwango kikubwa”.
Akamaliza kwa kusema: “Watekelezaji wa mradi huu ni shirika la ujenzi la ardhi takatifu, wameweka mkakati wa kukarabati milango yote ya Ataba tukufu, watakarabati mlango mmoja baada ya mwingine, upande wa nje na ndani”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya inatilia umuhimu mkubwa kazi ya kukarabati milango yote ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi hiyo ni sehemu ya mradi mkubwa wa upanuzi wa Ataba tukufu, hivyo milango inatakiwa itengenezwe kwa umaridadi na ujuzi mkubwa.