Atabatu Abbasiyya tukufu imejenga kituo cha kusafisha maji katika moja ya shule za Karbala

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha ujenzi wa kituo cha maji (R.O station) katika shule ya sekondari (upili) ya Abbasi (a.s), iliyopo mtaa wa Swamudi hapa Karbala.

Rais wa kitengo cha majengo ya kihandisi Mhandisi Samiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumejenga kituo hicho kutokana na maombi ya idara ya shule ya Abbasi (a.s) iliyopo katika mtaa wa Swamudi, baada ya tatizo la maji safi ya kunywa katika shule hiyo na wakazi wa mtaa huo”.

Akaongeza kuwa: “Kituo kimejengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa mita (40), kinauwezo wa kuzalisha lita (1000 kwa saa) na hodhi lake linaukubwa wa kutunza (lita 10,000)”. Akabainisha kuwa: “Katika ujenzi wa kituo hiki tumetumia mitambo yenye ubora wa kimataifa”, kasema kuwa tumefunga majokofu manne ya kupoza maji shuleni.

Uongozi wa shule ya Abbasi (a.s) umeshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi kwa kujenga kutuo hiki, wakasema kuwa hilo sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya kwani ipo mstari wa mbele daima katika kuhudumia watu wa Karbala.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imeshajenga miradi mingi ya kusaidia wananchi, miongoni mwa miradi hiyo, ipo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, changamoto kubwa ambayo tumekua mstari wa mbele kutatua ni ukosefu wa maji, tumeshajenga vituo vingi vya maji (R.O station) katika maeneo tofauti, maelfu ya watu wamenufaika na miradi hiyo, pamoja na mazuwaru na mawakibu zao, kuna vituo vilivyo jengwa rasmi kwa ajili ya kuhudumia watu wa ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: