Kuanza kuweka vioo kwenye paa la sardabu ya Imamu Jawaad (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza mradi wa kuweka vioo katika paa (dari) la sardabu ya Imamu Jawaad (a.s), ambayo ipo chini ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), upande wa mashariki katika eneo la katikati ya mlango wa Imamu Mussa Alkaadhim na Ali Alhaadi (a.s), lenye ukubwa wa (2m1,000) sehemu hiyo ni maalum kwa ajili ya mazuwaru wa kike.

Rais wa kitengo tajwa Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Uwekaji wa vioo ni miongoni mwa kazi zinazo pewa umuhimu na Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na umuhimu wa haram hii takatifu, pamoja na jinsi vioo vinavyo pendezesha, kazi hiyo inafanywa na mafundi wenye uzowefu mkubwa na uwezo wa kuowanisha ufundi wa zamani na wa sasa”.

Akaongeza kuwa: “Uwekaji wa vioo (maraya) ni kazi inayo hitaji umakini mkubwa, ujazo wake unafika (mlm 2) zinarangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuhimili mabadiliko ya mazingira, huwekwa kwa kutumia vifaa maalum sambamba na kuchagua rangi inayoendana na jingo tukufu la Ataba, aidha huwekwa kwa njia za kisasa”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi ya kuweka vioo inahitaji muda, kwani huhitaji umakini mkubwa na ufundi, sambamba na vipimo tofauti na wingi wa nakshi, kazi ya kubandika vioo ukutani hufanywa kwa mikono”.

Kumbuka kuwa Sardabu ya Imamu Hussein na Imamu Jawaad (a.s), ni miongoni mwa sehemu zilizo saidia kwa kiwango kikubwa kupunguza msongamano uliokuwa unashuhudiwa katika malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hususan wakati wa ziara, aidha zimesaidia sana upande wa wakinamama kwa kupunguza msongamano wao katika haram, kwani sardabu hizo zipo chini ya uwanja wa Haram mkabala na dirisha kwa ndani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: