Usanifu na ujenzi bora.. kazi inaendelea katika mradi wa ujenzi wa vitivo vya chuo kikuu kipya cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na ujenzi wa majengo ya vitivo vya chuo kikuu cha Al-Ameed, kilichopo katika eneo la Ibrahimiyya katika barabara ya (Baabil – Karbala), kama yalivyo sanifiwa kwa namna ambayo yanaendana na mahitaji ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa shirika linalo tekeleza mradi chini ya shirika la Lliwaaul-Aalamiyya wamefanya kazi kubwa katika kutekeleza mradi huu wa kimkakati, chini ya ufuatiliaji na usimamizi wa kitengo chetu, kazi kubwa imefanywa na mradi unatarajiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa”.

Akaongeza kuwa: “Kazi inaendelea vizuri katika sehemu zote, na ujenzi wa boma la juma upo hatua za mwisho”.

Akabainisha kuwa: “Jengo linaukubwa wa mita za mraba (1850) na linaghorofa nne na sehemu ya chini, kila ghorofa inakumbi mbili za madarasa na chumba cha maabara, chumba cha ofisi na cha kutolea huduma, aidha kuna ghorofa maalum la mkuu wa kitivo na taasisi zake pamoja na mambo yanayo hitajika katika jengo, kama vile umeme, viyoyozi, mawasiliano, intanet, zimamoto, tahadhari, kamera na mengineyo”.

Akaendelea kusema: “Kazi haijaishia hapo, bali kuna kazi zingine kwenye majengo mengine ya chuo, tumekamilisha msingi wa jengo la kitivo cha udaktari wa meno, na kazi ya uchimbaji wa kisima na usawazishaji wa kiwanja kwa ajili ya kujiandaa na ujenzi wa boma la chuma”.

Kumbuka kuwa mradi huu unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa dunam (40), panajengwa vitivo vya chuo, maabara zake na maabara kuu, jengo la mkuu wa chuo na lingine la maktaba kuu, na sehemu za bustani zitakazoweka mazingira mazuri ya usomaji, yanayo endana na malengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuanzisha miradi ya aina hii, na kuwa kitovu cha elimu katika mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: