Uzinduzi wa kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kulikarabati na kuweka vioo

Maoni katika picha
Alasiri ya leo siku ya Jumatano (22 Dhulqaada 1443h) sawa na tarehe (22 Juni 2022m), umefanywa uzinduzi wa kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kumaliza kulikarabati na kuweka vioo.

Msimamizi mkuu wa idara ya vioo katika kitengo cha ujenzi wa miradi ya kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Saidi Hassan Saidi Mahadi amesema: “Kazi hiyo imefanywa na watumishi wa kitengo chetu, ulikua ukarabati mkubwa kufanywa katika haram hii tangu miaka ya tisini karne iliyopita, imefanywa kwa ustadi mkubwa na kwa kufuata utaratibu uliowekwa, sambamba na kuweka mapambo yanayo endana na yale yaliyopo ndani ya haram tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Mapambo yaliyowekwa ni nakshi za kiislamu yanayo endana na nakshi zilizokuwepo zamani, pamoja na kuongeza urembo mwingine, vioo vilivyotumika vinaubora mkubwa na uwezo wa kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa”.

Tambua kuwa kazi hii ni sehemu ya ukarabati wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), unaofanywa chini ya utaratibu uliowekwa, unaoendana na utukufu wa sehemu hii, sambamba na athari za wazi kihandisi na kiufundi.

Kumbuka kuwa kazi zote zinafanywa na wahandisi na mafundi wa kiiraq miongoni mwa watumishi wa kitengo chetu, kazi inaendelea vizuri bila tatizo lolote wala kutatiza harakati za mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: