Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kipo katika maandalizi ya mwisho kuelekea ufunguzi wa Sardabu ya Imamu Aljawaad (a.s), ndani ya uwanja wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa kaskazini yenye ukubwa wa mita za mraba 1000.
Rais wa kitengo hicho Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi za kukamilisha mradi huu ni muhimu, nao ni mradi wa utoaji wa huduma ndani ya malalo takatifu, zimejumuisha uwekaji wa vioo vya rangi kwenye dari”.
Akaongeza kuwa: “Tumeweka pia marumaru za chini na ukutani sambamba na kuweka mapambo, nakshi na kuchora kwenye kuta za Sardabu, aidha tumetengeneza sehemu za kuweka misahafu, vitabu vya dua, vitabu vya ziara na turba”.
Akafafanua kuwa: “Sehemu ya juu ya ukuta imepambwa kwa maandishi ya Qur’ani yaliyo andikwa kwa hati ya Thuluth iliyoshiba kwa mkono wa Uastadh Ahmadi Naaji”.
Akasema: “Sardabu hiyo imewekwa pia mfumo wa viyoyozi ulio unganishwa na mfumo mwingine uliopo Ataba, kwa ajili ya kupoza hewa, hali kadhalika kuna mifumo ya (hewa – taa – umeme – tahadhari – ulinzi – vipaza sauti na zimamoto)”.
Akasisitiza kuwa: “Kukamilika kwa mambo hayo kunafungua milango ya kuongeza eneo hilo kwenye sardabu ya Imamu Hussein (a.s), itasaidia kupunguza msongamano ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuweka mazingira mazuri ya kufanya ibada kwa wanawake”.
Tambua kuwa mradi huu ni ujenzi wa chini ya haram ya malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), upande wa kaskazini katikati ya mlango wa Imamu Mussa Alkadhim na Ali Alhadi (a.s), nao ni miongoni mwa miradi yenye umuhimu mkubwa kwa Ataba tukufu kwa lengo la kuboresha huduma kwa mazuwaru, ujenzi huo umefanywa na watu waliobobea kwenye fani hiyo.
Kumbuka kuwa mradi unatekelezwa na shirika la ujenzi la Ardhi takatifu (shirika la kiiraq), chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ufadhili wa Wakfu-Shia.