Kikosi cha Abbasi kimerudi nchini na kuthibitisha kuwa kimekabidhi dirisha jipya kwenye malalo ya Aqiilah

Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kimekamilisha jukumu la kukabidhi dirisha jipya kwenye malalo ya Aqiilah-Zainabu (a.s) mbele ya jopo la mafundi wa Atabatu Abbasiyya waliopo kwenye malalo ya bibi Zainabu nchini Sirya.

Mkuu wa kikosi hicho Shekhe Maitham Zubaidi amesema “Tumekabidhi dirisha jipya la malalo ya kiongozi wa Sham kwa jopo la mafundi wa Atabatu Abbasiyya kutoka kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi na milango mitukufu”.

Akaongeza kuwa “Mwenyezi Mungu mtukufu amekiwezesha kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kutekeleza jukumu hili kwa baraka za Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani na maelekezo ya muwakilishi wake kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi”.

Akaendelea kusema “Temetekeleza ahadi tuliyotoa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, tumekabidhi amana takatifu ndani ya haram ya Zainabiyya mbele ya mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Kaadhim Abaadah”.

Dirisha tukufu liliwasiri jana siku ya Jumatano katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damaskas kutokea uwanja wa Ndege wa Najafu.

Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulikwenda sirya mapema kufanya makubaliano na viongozi wa Atabatu Zainabiyya tukufu, kuhusu utaratibu mzuri na gari zitakazotumika kubeba dirisha hilo kwa usalama ndani ya muda uliopangwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: