Kumaliza hatua ya pili katika ufungaji wa dirisha la kiongozi wa Sham ambayo ni kuunganisha vipande vya mbao

Msimamizi mkuu wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukufu katika Atabatu Abbasiyya bwana Huquqi Kaadhim Abaadah amesema kuwa wamekamilisha hatua ya pili ya kuunganisha dirisha la kiongozi wa Sham, kwa muda mfuoi sana, chini ya muda uliopangwa.

Akaongeza kuwa “Sehemu linapofungwa dirisha imewekwa marumaru za kifahari aina ya (Maltioksi) kutoka Italia, sambamba na kuweka mawe ya Aqiqi kutoka Yemen, jambo ambalo limependezesha sana eneo hilo na kufanya dirisha jipya kuwa na muonekano mzuri”.

Akasisitiza kuwa “Kazi ya ufungaji wa dirisha jipya inafanywa kama ilivyo pangwa, bali sehemu nyingi zinakamilika kabla ya muda uliotarajiwa, ikiwa ni pamoja na kuondoa marumaru za zamani na kuweka mpya”.

Naye mjumbe wa kamati ya mafundi Mhandisi Ali Salum amesema “Kazi haijaishia kwenye kufunga vipande vya mbao pekeyake, bali tumeanza kuweka vipande vyenye madini, tayali tumeweka kipande cha maandishi maalum ya ziara pamoja na ufito wa mapambo ya juu na tutaendelea kuweka vipande vingine baada ya kumaliza kazi hii”.

Akamaliza kwa kusema “Dirisha limetengenezwa kisasa na kwa ubora wa hali ya juu, zimetumika mbao bora zaidi kutoka (Burma)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: