Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika nchi ya Sirya ameenda kuangalia kazi ya ufungaji wa dirisha la bibi Zainabu (a.s)

Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika nchi ya Sirya Shekhe Abdulhalim Bahbahani ameenda kuangalia ufungaji wa dirisha jipya la malalo ya bibi Zainabu (a.s).

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi amesema “Hakika muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu amekua akitutembelea toka tulipoanza kazi ya kufunga dirisha jipya la malalo ya bibi Zainabu (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Katika ziara hii ameona hatua tuliyo fika na kazi kubwa inayofanywa na wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kutengeneza na kufunga dirisha hili”.

Akamaliza kwa kusema “Baada ya kututembelea, Mheshimiwa Shekhe Bahbahani amesifu kazi nzuri ya ufungaji wa dirisha na kawapongeza wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuwatakia mafanikio mema”.

Kazi ya ufungaji wa dirisha jipya la malalo ya bibi Zainabu (a.s) inaendelea vizuri na ipo katika hatua za mwisho, inatarajiwa kukamilika ndani ya muda mfupi, itakuwa tayali kwa uzinguzi ndani ya siku chache zijazo kama ilivyo pangwa Insha-Allah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: