Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi leo siku ya Jumapili amezindua Sardadu mbili ya Imamu Hussein na Imamu Jawaad (a.s).
Uzinduzi huo umefanywa sambamba na maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Ali (a.s), yaliyo hudhuriwa na rais wa uongozi wa wakfu Shia Dokta Haidari Shimri, mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Jaasim Naswifu Alkhatwabi na viongozi wengine, bila kumsahau katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ujenzi wa Sardabu unalenga kuongeza uwezo wa kuingia idadi kubwa ya mazuwaru, hasa wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, Sardabu ya Imamu Hussein (a.s) ipo chini ya ukumbi wa haram tukufu mkabala na uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Ukubwa wa Sardabu ya Imamu Hussein (a.s) ni (mt.66) urefu na (mt.14,2) upana, kuta zake zimepambwa kwa nakshi na marumaru, pamoja na kabati maalum za kuwekea misahafu, vitabu vya dua, ziara na turba, sehemu ya juu imezungushiwa ufito wa maandishi ya aya za Qur’ani.
Sardabu inajumla ya taa za mapambo (32) zilizo tengenezwa na kampuni ya (Jeki) aina ya (Martiza) zilizotiwa maji ya dhahabu huku dari likipambwa kwa vioo vya rangi za kumetameta.
Kuna mfumo mzuri wa viyoyozi ulio wekwa kwa umaridadi mkubwa, na kufanya sehemu hiyo kuwa nzuri kwa ibada ya ziara, aidha kuna mwanga mzuri, mfumo wa tahadhari, zima moto, ulinzi, vipaza sauti na lifti za umeme.
Sardabu ya Imamu Aljawaad (a.s) inaukubwa wa mita za mraba elfu moja, ni maalum kwa ajili ya mazuwaru wa kike tu, ipo chini ya ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), upande wa kaskazini katikati ya mlango wa Imamu Mussa Alkaadhim na Ali Alhadi (a.s).
Wasmamizi wa ujenzi wa hizo Sardabu mbili ni kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.