Wakfu Shia: Uzinduzi wa Sardabu mpya katika Atabatu Abbasiyya ni sehemu ya kukamilisha miradi ya utoaji wa huduma.

Rais wa Wakfu Shia Dokta Haidari Shimri amesema kuwa, uzinduzi wa Sardabu mbili ya Imamu Hussein na Imamu Jawaad (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, kunaonyesha ukamilifu wa miradi ya kuhudumia mazuwaru.

Shimri ameyasema hayo alipo hudhuria ufunguzi wa Sardabu hizo, akasisitiza kuwa “Hakika ufunguzi wa Sardabu hizi unaonyesha ukamilifu wa miradi ya kuhudumia mazuwaru katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani Sardabu hizi zinasehemu maalum kwa ajili ya wanawake, zitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza msongamano wa mazuwaru hasa wakati za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.

Akaongeza kuwa “Sardabu mpya zitasaidia sana mazuwaru kutoka kila kona ya dunia, ukizingatia kuwa ni sehemu yenye mandhari nzuru, tulivu na salama, aidha unaweza kuingia na kutoka kwa urahisi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: