Mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Alkhatwabi, amesema kuwa Sardabu ya Imamu Hussein na Imamu Jawaad (a.s) katika Atabatu Abbasiyya zinaubora mkubwa sana.
Mheshimiwa mkuu wa mkoa Alkhatwabi alipohudhuria ufunguzi wa Sardabu hizo amesema: “Hakika Sardabu hizi, zinaubora mkubwa sana, zimekidhi vigezo vya majengo ya chini na kufungwa mifumo yote muhimu kama vile, umeme, zima moto, viyoyozi, tahadhari na kuzifanya kuwa mahala bora pakufanyia ziara”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya inafanya juhudi ya kupanua eneo lake kwa kununua nyumba zinazo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuzibomoa kwa ajili ya upanuzi wa haram tukufu, matokeo ya upanuzi huo ndio haya leo tumeshuhudia ufunguzi wa Sardabu mbili ya Imamu Hussein na Imamu Jawaad (a.s), bado juhudi zinaendelea za kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.