Sayyid Swafi amezindua milango miwili katika Atabatu Abbasiyya na kutembelea mradi wa uwanja wa Ummul-Banina (a.s).

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amezindua milango miwili ya Ataba tukufu na kuangalia maendeleo ya mradi wa uwanja wa Ummul-Banina (a.s).

Uzinduzi wa mlango wa Imamu Ali na Imamu Aljawaad (a.s) umehudhuriwa na idadi kubwa ya wajumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu na marais wa vitengo vya Ataba, bila kusahau viongozi wa serikali ya Karbala.

Sayyid Swafi amesikiliza maelezo kwa ufupi kuhusu malighafi zilizotumika kutengeneza milango hiyo na aina ya utengenezwaji wake, sambamba na kulinda usanifu wa zamani, hivyo ni milango ambayo imezingatia ubora wa kisasa na uzuri wa kale, kazi hiyo imefanywa na raia wa Iraq chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya.

Kisha Muheshimiwa Sayyid Swafi akatembelea mradi wa uwanja wa Ummul-Banina (a.s) Jirani na Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia maendeleo yake.

Shirika la Ardh takatifu linalosimamia mradi huo, likaelezea maendeleo ya mradi na changamoto walizopata katika utendaji na jinsi walivyo zitatua.

Mradi wa uwanja wa Ummul-Banina (a.s) unaeneo lenye ukubwa wa (20,000) m2, na nisehemu ya upanuzi unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lengo la kuongeza wigo wa kuhudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: