Kupitia hafla ya ufunguzi.. Sayyid Swafi ametangaza misaada ya chupa za maji ya dripu kwa taasisi za afya Palestina na Lebanon

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ameongea kuhusu misaada ya vifaa-tiba kwa taasisi za afya nchini Palestina na Lebanon.

Ufuatao ni ujumbe aliotoa wakati ya ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza chupa za maji ya dripu chini ya Ataba tukufu mkoani Karbala:

Watukufu wageni rasmi na wote mliohudhuria, Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu na Baraka zake.

Miongoni mwa mambo ambayo Atabatu Abbasiyya inayapa kipaombele zaidi, ni mambo mawili muhimu, sekta ya elimu na afya, maendeleo yanategemea kwa kiasi kikubwa sekta hizo mbili muhimu.

Alhamdulilahi kwa miaka mingi tumejikita katika utoaji wa huduma za kielimu, tumejitahidi kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi kuanzia masomo ya awali, msingi, sekondari hadi chuo, maelfu ya wanafunzi wamehitimu katika ngazi hizo, bado tunaendelea kuboresha na kupanua wigo zaidi katika sekta ya elimu kwa kufuata viwango vya kimataifa, tunamshukuru Mwenyezi Mungu shule zetu zimefikia viwango vinavyo hitajika kwa kiasi kikubwa, hii inatokana na kuweka mazingira mazuri ya walimu na wanafunzi.

Kuhusu sekta ya afya na matibabu, tumekuwa tukifanya kazi kubwa kuboresha sekta hiyo, taifa hili linastahiki kila kitu, kila tukipata nafasi tunaongeza juhudi, umuhimu wa tiba upo kila siku, tumekuwa tukifungua hospitali na hivi karibuni tunatarajia kufungua hospitali kubwa katika mkoa wa Baabil, tulikuwa na changamoto kidogo ya upungufu wa pesa, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tunatarajia kuvuka changamoto hiyo na kukamilisha mradi huo.

Miongoni mwa miradi ya sekta ya afya ni mradi huu, tulianza kuutekeleza wakati mgumu sana, wakati taifa lilipokua katika changamoto ya magaidi wa Daesh, jambo hilo lilisababisha kuchelewa ukamilishwaji wake, kuchelewa kwetu pia kumetupa nafasi ya kufanya tafiti zaidi kuhusu kujifunza maendeleo ya kielimu ya viwanda vya kutengeneza chupa za maji ya dripu, wahandisi na madaktari wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kiwanda hiki kinakidhi vigezo vya kimataifa, baada ya kumaliza mazungumzo yangu tutatembelea baadhi ya maeneo ya kiwanda Inshallah, ili mjionee kazi iliyofaywa katika ujenzi wa kiwanda hiki.

Kila mtu anajua mahitaji ya viwanda vya kutengeneza chupa za maji ya dripu, yanahitajika kila siku, kwa mujibu wa takwimu ya idara ya afya, Iraq inahitaji zaidi ya chupa za nusu lita milioni 120 kwa mwaka, hakika hichi ni kiwango kikubwa, kiwanda hiki kinauwezo wa kutengeneza chupa milioni 27 kwa mwaka, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutaanza kuingiza sokoni bidhaa zetu.

Tunawashukuru wote mliokuja kutuunga mkono katika siku ya leo kwenye ufunguzi huu, tunawashukusu sana watu wote waliofanya kazi kubwa ya kufanikisha mradi huu muhimu kwa huduma za watu.

Tunawakumbusha kuwa leo dunia inapitia matatizo makubwa sana, hususan raia wa Palestina na Lebanon, nchi hizo zinashambuliwa vikali na utawala haram wa kizayuni. Watu wengi wanauawa na kujeruhiwa kila siku, jambo ambalo limeongeza kwa kiwango kikubwa sana mahitaji ya chupa za maji ya pripu na vipaa-tiba vingine, tumefanikiwa kukusanya chupa laki mbili na elfu hamsini kwa ajili ya kusaidia raia wa Palestina na idadi kama hiyo kwa raia wa Lebanon, misaada hiyo tumetoa kupitia wizara ya afya la Iraq, kwani ndio sekta rasmi inayowasiliana na mataifa hayo.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiwezeshe wizara ya afya kufikisha misaada hiyo kwenye mataifa hayo, ama wale waliokuja hapa nchini kwetu sisi tunawapa huduma zote zinazohitajika kwao.

Mwisho tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwezeshe kutumikia taifa hili na awaponye haraka majeruhi, jambo hilo ni jepesi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: