Wageni washiriki wa hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza chupa za dripu wametembelea maeneo tofauti ya kiwanda hicho

Wageni washiriki wa hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza chupa za dripu za dawa chini ya Atabatu Abbasiyya, wametembelea maeneo tofauti ya kiwanda hicho.

Wamefanya hivyo baada ya hafla ya ufunguzi iliyohudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi ya viongozi wa Ataba na viongozi wa kidini na kijamii kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Kiwanda cha Aljuud kinavifaa-kazi bora kutoka makampuni makubwa ya kimataifa, kinazalisha zaidi ya aina 24 za chupa zenye mchango mkubwa katika sekta ya vifaa-tiba na idara ya afya kwa ujumla hapa nchini.

Jioni ya Jumatano, Atabatu Abbasiyya imezindua kiwanda cha kutengeneza chupa za dripu za dawa katika mkoa wa Karbala, chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi na ufadhili wa Ataba tukufu, kiwanda hicho kinatarajiwa kutengeneza chupa milioni 27 kwa mwaka, kitasaidia kupunguza tatizo la chupa hizo hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: