Mhandisi Hussein Muhammad Baaqir amesema “Watumishi wetu wameanza kazi ya kuweka sakafu kwenye ukumbi wa Sardabu ya Ummul-Banina (a.s) yenye ukubwa wa mita za mraba 340, hadi sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80%”.
Akaongeza kuwa “Eneo linahusisha vyumba na kumbi, pamoja na vyumba vinavyotumika kwa ulinzi, mradi unatekelezwa kwa kufata mchoro na usanifu wa awali”.
Mtendaji mkuu wa mradi ni shirika la ujenzi (Ardhi takatifu) shirika la kiiraq, kwa ufadhili wa uongozi wa Wakfu-Shia, baada ya kukamilika mradi huo utaweza kuingiza idadi kubwa ya mazuwaru na kupunguza msongamano, sambamba na kuwahudumia.