Rais wa kitengo Sayyid Nadhim Ghurabi amesema “Watumishi wa kitengo wanaendelea na kazi ya kufunga dirisha la Sardabu ya Imamu Hussein (a.s), lililopo chini ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inahusisha uwekaji wa sehemu za madini kwenye dirisha, baada ya kukamilisha kufunga sehemu za mbao”.
Akaongeza kuwa “Kazi iliyobaki ni kuweka baadhi ya sehemu ndogo, kwa ajili ya kujiandaa na upokeaji wa dirisha kamili siku chache zijazo”, akasema kuwa “Dirisha limetengenezwa ndani ya karakana maalum za kitengo na raia wa Iraq wabobezi”.
Akabainisha kuwa “Kitengo kinazingatia kukamilisha kazi kwa ubora na ustadi mkubwa, iliyodumu kwa muda unaokaribia miaka miwili, ambayo imefanywa kwa vifaa vya kisasa zaidi katika sekta ya utengenezaji wa madirisha ya makaburi”.