Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya ametembelea kiwanda cha Nuur cha utengenezaji wa panel za umeme wa jua

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ametembelea kiwanda cha Nuur cha utengenezaji wa panel za umeme wa jua.

Katika matembezi hayo, Muheshimiwa amefuatana na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, amesikiliza maelezo kwa kina kuhusu mafanikio ya kiwanda hicho.

Muheshimiwa Sayyid Swafi amepongeza kazi nzuri inayofanywa na kiwanda hicho, akawataka waongeze juhudu na kuwatakia maendeleo mema.

Kiwanda kinazalisha bidhaa za umeme wa jua kwa ajili ya shirika la umeme la Alkafeel, nacho ni kiwanda cha pekee hapa Iraq na kinatengeneza bidhaa zenye ubora mkubwa.

Kiwanda kimefikia viwango vya juu katika uzalishaji wa vifaa vya umeme, kina mchango mkubwa katika utoaji wa ajira na kusaidia uchumi wa taifa.

Atabatu Abbasiyya inaendelea kuboresha miradi ya umeme na kuimarisha sekta ya elimu, viwanda na kilimo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: