Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya amekagua utendaji wa kazi katika kiwanda cha Nuru cha kutengeneza panel za sola

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amekagua utendaji wa kiwanda cha Nuru cha kutengeneza panel za sola, ili kufuatilia maendeleo ya kiwanda hicho.

Sayyid Swafi amefuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Ataba tukufu, Mhandisi Dhiyaau Swaigh na baadhi ya wahandisi na mafunzi.

Muheshimiwa amekagua hatua za uzalishaji, kuanzia utengenezaji wa vifaa vya awali hadi kazi ya ukusanyaji, upembuzi na udhibiti.

Ziara hiyo imehusisha ufuatiliaji wa mnyororo wa uzalishaji na kuangalia mazingira halisi ndani ya kiwanda kwa kuzingatia vipimo na ubora wa bidhaa.

Mradi huo unatokana na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuimarisha sekta ya nishati kwa kutegemea nishati mbadala na kupunguza utegemezi wa umeme wa kawaida.

Kiwanda cha Nuru ni moja ya miradi ya viwanda vinavyo endeshwa na Ataba tukufu, chini ya mkakati wa harakati za kihandisi zinazolenga kusaidia shughuli za kuhudumia zuwaru na kutumia teknolojia za kisasa katika kuboresha utoaji wa huduma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: