Picha baada ya kukamilika kwa ukarabati na uwekaji wa marumaru: Ukuta wa nje wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vazi jipya..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshuhudia miradi mingi, miongoni mwa miradi hiyo ni kukarabati kwa jengo la malalo matukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wahandisi mahiri wametekeleza makumi ya miradi ya ukarabati, miongoni mwa miradi hiyo ni huu wa kukarabati ukuta wa nje wa haramu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao upo ndani ya miradi ya upanuzi wa haram tukufu na upauaji wa uwanja wake.

Kazi zilifanyika kwa kufata ratiba iliyowekwa na shirika la Almunqidha nalo ni shirika la Aridhi tukufu la ujenzi, chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, rais wa kitengo hicho aliiambia Alkafeel kua: “Mradi huu uligawika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza: Upande wa magharibi mkabala na milango miwili, mlango wa imam Hussein na Swahibu Zamaan (a.s). Sehemu ya pili: Upande wa kusini mkabala na mlango wa imam Jawaad (a.s). Sehemu ya tatu: Upande wa mashariki mkabala na mlango wa Furaat (Alqamiy)”.

Aliendelea kusema kua: “Mradi umepitia hatua nyingi hadi kufikia muonekano huu wa mwisho, miongoni mwa hatua hizo ni:

Kwanza: Kutoa Kashi karbalaai (mapambo yenye nakshi) za zamani pamoja na ripu hadi kuzifikia kuta za asili.

Pili: Kukarabati sehemu zenye mipasuko kwa kutumia zana maalumu za kisasa.

Tatu: Kuimarisha ukuta wa asili kwa kuongezea ukuta saidizi wenye sehemu ya chuma na kwa unene maalumu kutokana na umuhimu wa ukuta halisi.

Nne: Kuweka nyaya maalumu za umeme na vipaza sauti na kuziunganisha na zile za uwanja wa haram tukufu.

Tano: Kuweka vipande vya madini ya (haarib) katika kuta kwa ajili ya kushikishia Kashi.

Sita: Kuweka Kashi karbalaai, aina ileile iliyotumika katika kuta za korido za uwanja wa haramu tukufu kwa ajili ya kupendezesha muonekano wake”.

Aliendelea kufafanua kua: “Kwa kukamilika mradi huu, tunakua tumemaliza hatua muhimu inayo ingia katika hatua zingine zilizo kamilika katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika utekelezaji wa mradi huu tumezingatia na kuchunga mambo mengi hasa katika umaliziaji, tumeweza kuweka muonekano mzuri wa kihandisi wenye uwiano na sehemu zingine za uwanja wa haram tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: