Kwa picha: Muendelezo wa uwekaji wa mapambo na nakshi za kiislamu katika kubba za Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa dani..

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza matengenezo ya upande wa mbele katika mlango wa kibla wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi imehamia upande wa ndani wa mlango huo kwa kuweka nakshi na mapambo, huu ni miongoni mwa milango muhimu inayo tumika kuingia katika uwanja wa haram tukufu, na Atabatu Abbasia kupitia kitengo cha miradi inaupa umuhimu mkubwa kutokana na nafasi yake kwa mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo cha uhandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao ndio wasimamizi wakuu wa utekelezaji wa mradi huu alisema kua: “Mradi wa upanuzi wa milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kupanua milango ya zamani hadi kufikia mita (11) upana na urefu, na sasa hivi kazi ipo katika hatua ya mwisho upande wa ndani ambapo zinawekwa kashi karbalaai aina sawa na ile iliyopo katika kuta za Ataba tukufu kwa ajili ya kuweka mandhari nzuri na kuzipamba kwa nakshi za dhahabu kama zilizo kuwepo zamani, zinazo fanana na zile zilizopo ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Nakshi na mapambo ya milango hii zilikua ni nusu duara sita zenye ufito wa dhahabu na kashi karbalaai, zimeongezwa nusu duara tatu zenye ufito wa dhahabu na kuna maandishi ya aya za Qur an, mapambo ya fito za dhahabu yanafika hadi kwenye dari la ndani la mlango huo, mapambo hayo yapo pande zote mbili za mlango”.

Akabainisha kua: “Kazi ya kufunika kuta hizi ilitanguliwa na kazi ya kuzisafisha na kuzisawazisha kisha kuweka vitu maalumu vinavyo saidia kushikisha kashi karbalaai pamoja na vitu vingine”.

Kumbuka kua miongoni mwa vipengele vya mradi huu vinaingia katika mradi mkubwa wa upanuzi wa Ataba tukufu, ambao unajumuisha upanuzi wa milango ya zamani na kuifanya iweze kubeba idadi kubwa wa watu wanaokuja kufanya ziara na misafara ya Husseiniyya ya kudumu, pamoja na kuiwekea mapambo ya nakshi za kiislamu kutokana na plani ya kila mlango, milango hii imeplaniwa na kutengenezwa na shirika la aridhi tukufu la ujenzi na kusimamiwa moja kwa moja na kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na yanayo husiana na milango hiyo ikiweme, mapambo na maandishi na nakshi hivyo ilihitaji muda kukamilika kwa kazi hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: