Mradi wa matangazo ya moja kwa moja (SNG) kutoka ndani ya Atabatu Abbasiyya wafikia hatua za mwisho..

Maoni katika picha
Mradi wa matangazo ya moja kwa moja (SNG) kutoka ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umefikia katika hatua za mwisho baada ya kukamilika sehemu kubwa ya ufungaji wa mitambo.

Mradi unahusisha kamera kumi na moja (Motorized Camera) zinazo fungwa katika maeneo tofauti ya Ataba tukufu na zitatumiwa kwa mbali, pia kutakua na kamera zingine tano zinazo zunguka na kurusha picha katika (SNG) ya kisasa zaidi.

Mradi huu unalenga kurusha harakati zote zinazo fanyika ndani ya Ataba tukufu, kama vile: (swala za jamaa na ibada zingine, pamoja na makongamano, mikutano, majaalisi za huzuni, na mengineyo) na yatarushwa na vifaa vya kisasa zaidi vyenye sifa za kimataifa.

Hali kadhalika mradi huu unalenga kusaidia vyombo vya habari ambavyo havija weza kuleta mtu wao ndani ya Ataba tukufu wakati wa tukio, pia kutakua na masafa maalumu ya Ataba itakayo rusha harakati zote bila ya kuwepo kwa wanahabari wao ndani ya Ataba, jambo la muhimu zaidi ni kutoa huduma bora inayo endana na hadhi ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika nyanja zote.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kufanya upembuzi yakinifu pamoja na watu watakao tekeleza mradi huu, nao ni idara ya wapiga picha na wa andaaji wa vipindi, chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia uwezo wao katika swala hili, tulifanya makubaliano na moja ya shirika linalo fanya shughuli hizi, na tukaunda kamati itakayo simamia mradi huu, tukawapa mamlaka ya kusimamia vifaa, kisha zika ainishwa sehemu zitakazo husishwa katika mradi ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni pamoja na kubaini urefu wa nyaya zitakazo tumika, vikaandaliwa vifaa vyote vinavyo hitajika katika mradi, kama vile nyaya, kamera pamoja na mtambo wa (SNG)”.

Naye ustadh Bashiri Taajir kiongozi wa idara ya wapiga picha na waandaaji wa vipindi ambao ndio watakao simamia mradi huu, alisema kua: “Mradi utahusisha kamera kumi na moja zitakazo fungwa katika maeneo tofauti ndani na nje ya uwanja wa haram tukufu, pia kutakua na kamera za kubeba zikiwemo kamera tano za kuzunguka ambazo zinaendeshwa kwa mbali, kutoka katika chumba cha uongozaji wa mitambo (ulinzi), na yataundwa masafa maalumu kutoka katika kifaa cha (SNG), kupitia masafa hayo itawezekana kurusha matangazo ya moja kwa moja katika vyombo vya habari vitakavyo penda kurusha matangazo hayo kutoka ndani ya haram takatifu ya Abbasi na kushuhudiwa na waislamu pamoja na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka katika sehemu hii tukufu kwa mara ya kwanza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: