Pamoja na kukaribia ufunguzi wake: Zifahamu hatua muhimu za mradi wa upanuzi wa haram katika upauaji wa ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Kutokana na ramani za usanifu wa mradi wa upanuzi wa haram katika kupaua ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambao ufunguzi wake umekaribia, ujenzi huo ulipitia hatua nyingi, zifahamu hatua zake muhimu:

  • 1- Hatua ya usanifu wa jengo:

Baada ya kupasishwa kwa usanifu wa jengo, ambayo ni sehemu muhimu sana kwa mujibu wa fani za kihandisi, kwa sababu ndio hatua ya kwanza inayo tuwezesha kuingia katika hatua ya pili (hatua ya utekelezaji wa mradi), kutokana na umakini wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kutaka jambo hili liende pamoja, baada ya kupasishwa kwa usanifu wa jengo na usanifu wa utekelezaji nao ukakamilika, kwa sababu vilitengenezwa kwa pamoja.

  • 2- Hatua ya usanifu wa utekelezaji:

Ni usanifu wa sehemu zote za jengo, miongoni mwa sehemu hizo ni:

  1. Usanifu wa nguzo za zege zilizo kua zimezunguka haram ya zamani, na usanifu wa nguzo mpya zinazo shikilia paa na kuongeza uimara kwa kuweka vyuma.
  2. Sehemu zote za paa zimejengwa kwa vyuma (Sandwich Panel).
  3. Mazingira ya paa yaliandaliwa kwa kuezekwa na (Sandwich Panel).
  4. Kuweka sehemu za vioo katika paa na madirisha ya kubba la pili, kwa kutumia aina ya (Sky light) inayo muwezesha mtu aliyopo ndani kuona sehemu ya anga kwa kutumia vifuniko vinavyo tembea (slide), vimetumika vioo bora zaidi na uimara mkubwa kutokana na wasifu wake wa kihandisi, na vimewekwa katika sehemu inayo tembea (Slide) katika mradi huu.
  5. Usanifu wa vifaa tumishi: (AC, feni, mataa, mawasiliano, spika, mpangilio ya vifuniko vya vioo, usambazaji wa maji, ma vinginevyo).

  • 3- Hatua ya utekelezaji:

Waliingia mikataba na shirika la Aridhi tukufu la ujenzi, kama watekelezaji wa mradi huu, na wakaweka mashariti ya kihandisi na kiujenzi katika maeneo yote kama vile katika maswala ya umeme na vinginevyo, na kuchagua mashirika mengine yatakayo tengeneza vitu ambavyo havita tengenezwa na shirika hilo, maadam utendaji wao na ubora wao ufanane na shirika kuu lililo pewa kazi ya kutekeleza mradi.

Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndio wasimamizi wakuu katika sekta zote za mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: