Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu (idara ya uandaaji wa vipindi na matangazo ya moja kwa moja) imetangaza kukamilika kwa maandalizi ya chanel itakayo rusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe za uzinduzi wa mradi wa upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa upauaji, zitakazo fanyika leo siku ya Juma Mosi jioni baada ya swala ya Isha.
Wametoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa vitakavyo taka kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hiyo itakayo anza saa moja na nusu leo jioni, wafatilie katika masafa zifuatazo:
EUTELSAT 3B
Down 11,025.9620 H
SR 3,300
Fes 3/4
Dvbs2-HD
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Ustadh Bashiri Taajir kiongozi wa ofisi hiyo na namba (009647706007187) au unaweza kuwasiliana na Muhandisi Ihaabi Al-awidi kwa namba (009647706054144) katika Ataba tukufu.