Mtandao wa Alkafeel wa kimataifa unakuletea picha za mradi wa upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika upande ya upauaji wa uwanja wa haram tukufu, ambao sherehe za uzinduzi wake zitaanza saa moja kuto sasa, katika eneo la mkabala na mlango wa Qibla ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Haya ni matunda ya juhudi halisi za wairaq katika nyanja ya uhandisi na uongozi (utendaji na idara), kazi hii imedumu kwa muda wa miaka miwili kuanzia usanifu wa jengo na utekelezaji wa mradi chini ya wataalamu wa Ataba tukufu, wairaq wamefaulu kwa kusimamia usanifu na utekelezaji wa mradi huu, wamekamilisha kazi iliyo anzwa na babu zao, walio jenga haram mbili tukufu ya Husseiniyya na Abbasiyya katika mwaka wa (767 h) wakati wa utawala wa Jalairiyya Almaghuliyya, wameweka katika akili zao na juhudi za ubunifu wa tamaduni za kiiraq ulio dumu karne (67).