Sayyid Ahmad Swafi
Yafuatayo ni mambo muhimu aliyo ongea katika hotuba yake:
- 1- Katika usiku huu mtukufu wa kukumbuka kuzaliwa kwa bibi kipenzi chetu Fatuma (a.s) Radhiyya Mardhiyya Hauraa Insiyya Swiddiqah Shahidah, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu kwa baraka zake na kwa baraka za baba yake na mumewe na watoto wake na siri iliyopo kwake akupatieni wote kwa ujumla amani na usalama na afya njema na anawirishe macho yetu sote kwa kumuona mjukuu wake imamu Almuntadhir (a.f) na ifanyike haraka kumnusuru.
- 2- Katika usiku huu kuna ushindi umepatikana katika vita wanayo pigana wairaq watukufu, wanailinda aridhi hii takatifu kwa miili yao na damu zao, wanaandika historia ya utukufu, wanashindana katika kujitolea kwao kwa ajili ya kuhifadhi utukufu wa nchi hii, na kuitikia fatwa tukufu iliyo tolewa na muheshimiwa Sayyid Sistani (M/M arefushe umri wake mtukufu), damu tukufu iliyo mwagika katika aridhi na bado inaendelea kumwagika, tunamuomba Mwenyezi Mungu kutokana na ushindi unao patikana, atupatie haraka utukufu, amani, usalama na utulivu.
- 3- Tumefurahishwa sana na muitikio wenu wa kuhudhuria uzinduzi wa mradi huu mtukufu wa upauaji wa uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), nao ni mradi unao kamilisha upanuzi wa haram katika upande wa nje, mimi sitaki kuuelezea mradi kwa kina, kwa sababu wataongea wasanifu na watekelezaji wa mradi, huenda watafafanua mambo yanayo hitaji kufafanuliwa, lakini nitazungumzia nukta mbili kwa haraka haraka.
Nukta ya kwanza: Huu mradi uliopo mbele yetu sasa hivi, katika hatua ya usanifu, ulituchukua karibu miaka miwili, kwa sababu usanifu ndio msingi wa mradi, ilikua kuna mambo muhimu lazima yapatikane katika mradi huu, miongoni mwa mabo hayao ni kuhakikisha uwanja wa haram unabakia bila nguzo yeyote kutokana na udogo wa eneo lake, Alhamdu lilahi usanifu ulikua unaweza kutekelezeka ndio tumepata hiki mnacho kiona mbele yenu.
Nukta ya pili: Tumejaribu kufanya mradi huu wa upauaji ufanane na paa la Haram tukuhu kwa ndani kwa kutumia njia maarufu hivi sasa ambayo ni njia ya kutumia vioo, na kuvigundisha kwa kutumia Jibsi, yalipo fanyika mahesabu ya kihandisi ikaonekana tunahitaji tani (75) za Jibsi ili vioo vibandikwe juu yake, uzito huo ni mkubwa sana haufai kubebwa, tukachagua njia nyingine ambayo inauzito mwepesi na imara zaidi, ambayo ni kutumia (Viber Grass) vina uimara mkubwa na uzito mdogo navyo vilitengenezwa nchini Malesia, tukaitumia njia hii kwa ajili ya kupunguza uzito, kwa kweli tunathamini sana juhudi za wasanifu na za ndugu zetu kitengo cha miradi ya kihandisi, hakika wamefanya juhudi kubwa sana hadi paa hili kua hivi lilivyo, vioo hivyo viliwekwa kwa umakini wa hali ya juu kabisa, walikua wanachukua vipimo wanavituma katika mashirika na wanafuatilia, hakika vifaa vyote vilivyo kuja vinaendana na usanifu wao, hatukupata tabu tulipo anza kuweka miamba (mitambaa panya) ya chuma, na kazi hiyo ilianza mwezi wa Ramadhani mtukufu.
- 4- Nawabainishia ndugu wapenzi na kila anaye taka kufahamu baadhi ya mambo, sisi tulipewa jukumu la utumishi wa Ataba hii mwaka (2003 m) na sasa hivi tupo katika mwaka wa (2017 m) tunasema: Jumla ya pesa iliyo tumika katika miradi ya ujenzi na miradi ya kiutumishi ya Ataba tukufu ndani ya miaka (13) zinafika dola bilioni moja, tukigawa pesa hizo kwa kila mwaka itakua sawa na tumetumia dola milioni (76) kila mwaka, fahamu kua Ataba tukufu ina zaidi ya miradi (150) na bado kuna miradi mingine (40) ipo katika hatua ya usanifu na imesimama kwa sababu ya matatizo ya kipesa, na baadhi ya miradi imepasishwa na wakfu shia inasubiri ruzuku.
- 5- Natoa shukrani kwa ndugu wote watukufu ambao wamesaidia kufanikisha kwa miradi hii, hasa uongozi wa wakfu shia katika idara zake mbili, idara ya Sayyid Haidariy na idara na ngugu yangu kipenzi Sayyid Alaa Mussawiy (M/M awape amani) pamoja na ngudu watukufu wa idara ya Ataba, wamefanya kazi kubwa sana, hakika miradi hii imekamilika kutokana na kujitolea kwao, hususan ndugu yangu mtukufu Sayyid Muhammad Ashiqar alipokua naibu rais wa kitengo cha Uhandisi, kisha kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu sasa hivi amekua katibu mkuu wa Ataba tukufu, naye ni kiongozi bora kabisa.
Na mwishowa maneno yake Sayyid Swafi alisema: “Ninawashukuru ndugu zangu wapenzi watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kwa juhudi kubwa mnazo fanya katika kuendeleza Ataba hizi hususan ndugu yangu muheshimiwa Shekh Karbalai (M/M ampe amani na afya) katika kuitumikia Atabatu Husseiniyya tukufu, na Atabatu Alawiyya, Kadhimiyya Ataba zote sasa hivi zina maendeleo makubwa katika uboreshaji wa majengo na huduma kwa msaada wa uongozi mtukufu wa wakfu Shia, namuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awadumishe katika taifiq yake.
Pia napenda kuwashukuru wapiganaji wote walio kua nyuma ya pazia walio saidia kufanikisha kwa mradi huu na miradi mingine sawa iwe katika mashirika yaliyo tekeleza miradi au katika mawasiliano mbalimbali yaliyo kua yanalenga kufanikisha kwa mradi huu, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atufunike daima katika kivuli cha rehema zake na paa ya maimamu watakasifu (a.s) hususan bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ni utukufu ulioje! Kufunikwa na kivuli chake daima hususan katika kisimamo tutakacho simama wote katika siku ya kiyama.. Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwezeshe kujiandaa ili tuwe miongoni mwa watu ambao watachaguliwa na kutolewa motoni kama ndege anavyo chagua mbetu za mtama”.