Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majid Swaaigh ametangaza kukamilika kwa hatua ya pili na ya mwisho katika mradi wa kuweka dhahabu katika minara ya malalo ya Sayyid Muhammad mtoto wa imamu Ali Haadi (a.s), mradi huu umetekelezwa na wairaq na umefanywa kwa umaridadi mkubwa na ufanisi wa hali ya juu, kuanzia katika kutengeneza vifuniko vya dhahabu hadi namna vilivyo wekwa, bali ufanisi wa kazi hii unazidi kazi nyingi zilizo fanywa na mashirika ya kimataifa.
Akaongeza kusema kua: “Uzinduzi wa mradi huu utafanyika siku ya Juma Tano (27 Shabani 1438h) sawa na (24 May 2017m), siku hiyo itafunguliwa pazia katika hafla itakayo fanyika kwenye ukumbi wa haram ya Sayyid Muhammad (a.s), jambo hili litathibitisha wazi uwezo wa wairaq katika kutekeleza miradi ya aina hii, ambayo imekamilika kwa muda muwafaka na kwa ubora wa hali ya juu”.
Akaendelea kuelezea hatua za utekelezaji zilizo fanywa katika mradi huu: “Uwekaji wa dhahabu katika minara ya Sayyid Muhammad (a.s) ulipitia hatua kadhaa, hatua ya kwanza ilikua kuweka dhahabu sehemu ya juu ya minara, ambayo ni sehemu ya mshumaa na taji (kofia), pamoja na chumba cha muadhini sambamba na aya za Qur’an za surat Nuur, sehemu hizo zilitiwa dhahabu na madini ya mina ya moto, hatua ya pili; ilihusisha maandishi ya aya za Qur’an yaliyo chukua vipande (18) vya vifuniko vya madini yaliyo tiwa dhahabu na mina ya bluu kutoka katika surat Anbiyaa, ambazo ni: (Na hakika tuliandika katika Zaburi baada ya ukumbusho kuwa: Ardhi (hii) watairithi waja wangu walio wema * Hakika katika haya kuna ujumbe kwa watu wafanyao ibada * Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu).
Ambazo zimeandikwa kwa hati ya muiraq Farasi Abbasi, jumla zimetumika (kg 8) za dhahabu katika maandishi hayo, yanaurefu wa (mt 11) na ukubwa wa herufi ni (mt 1.40) herufi hizo zimezungukwa na mstari wa dhahabu juu na chini ambao umetiwa madini ya mina pia, mistari yote wa juu na chini imetengenezwa kwa vifuniko ya dhahabu”.
Akaongeza kusema kua: “Hatua hii vilevile ilijumuisha upambaji wa minara hiyo kwa Kashi Karbalai zilizo tiwa dhahabu ambazo ni nzuri na imara zinastahamili mazingira magumu zenye urefu wa (mt 8.60) zenye nakshi nzuri zinazo endana na nakshi zingine za haram tukufu, kila mnara umeandikwa majina ya maimamu maasumina (a.s), kwa ufupi minara hii imetengenezwa kwa umaridadi na ustadi wa hali ya juu kabisa kuanzia juu hadi chini”.
Akafafanua kua: “Jumla ya dhahabu halisi iliyo tumika katika mradi huu ni kilo (25) na madini ya aina zingine yalifika kilo (2268), vifuniko vya dhahabu vilitengenezwa kwa mikono na mafundi wa idara ya dhahabu chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi kwa kutumia ngozi ya swala”.
Kumbuka kua mradi wa utiaji dhahabu katika minara ya malalo ya Sayyid Muhammad (a.s) ndio mradi wa kwanza wa aina hii kutekelezwa nje ya Atabatu Abbasiyya, baada ya mafanikio yaliyo patikana katika mradi wa uwekaji dhahabu katika minara ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ulio tekelezwa kwa asilimia mia moja (%100) na mafundi wa kiiraq.